Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MANYARA: TAKUKURU yapokea malalamiko 67 ya wananchi

Manyara Pic Data Takukuru Manyara yapokea malalamiko 57 ya wananchi

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Manyara imepokea malalamiko 57 ya uchunguzi wa mashtaka katika kipindi cha miezi mitatu.

Akizungumza leo Februari Mosi, 2022 mjini Babati, mkuu wa Takukuru wa mkoa huo, Holle Makungu amesema kati ya malalamiko hayo 57, malalamiko 19 yanahusiana na rushwa.

Makungu amesema malalamiko matano yanahusiana na idara ya elimu kwenye halmashauri zote saba za mkoa huo na malalamiko dhidi ya polisi ni matatu.

Amesema malalamiko 33 ni dhidi ya wenyeviti, watendaji wa vijiji na kamati mbalimbali za vijiji, idara ya afya malalamiko manne, watu binafsi na mashirika binafsi manne.

Mkuu huyo amesema wamepokea malalamiko matatu idara ya mahakama na mengine matatu dhidi ya mashirika ya dini moja, vyama vya ushirika, wakala wa barabara za vijijini na mijini (Tarura) na idara ya maliasili.

“Kati ya malalamiko hayo 57, malalamiko 19 hayahusiani na vitendo vya rushwa, hivyo wahusika walishauriwa ipasavyo na yale yanayohusu rushwa yapo kwenye hatua ya uchunguzi,” amesema Makungu.

Amesema katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka jana, kesi nane zimefunguliwa mahakamani na kufanya jumla ya kesi zilizofikishwa mahakama kuwa 33.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live