Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAITI YA MTOTO YAZUA TAHARUKI, WANANDUGU WAGOMBANIA

ZENJIBAR Copy 2 2?fit=800%2C445 MAITI YA MTOTO YAZUA TAHARUKI, WANANDUGU WAGOMBANIA

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Katika hali isiyo ya kawaida familia mbili zimejikuta zikiingia kwenye mzozo kubwa baada ya kugombania maiti ya mtoto na huku baadhi yao wakiwa na mapanga mikononi na wengine kukikmbia kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea huko Mbuzini Mkoa wa Mjini Magharib Unguja ambapo mama mzazi wa mtoto huyo alisema walikubaliana na mumewe kuwa mtoto atazikwa upande wa mama yake ila anashangaa kuona ndugu wa mumewe wakija na kufanya fujo mazikoni hapo .

“Naombo serikali inisaidie mwanangu kadhalilishwa sana, mimi ndo nilokuwa namlea mwanagu nimehangaika nae kapata ajali 8 kazama kwenye maji mara moja kapotea mara 4 sijapata ushirikiano wa mtu saiv kafa watu wanachukua maiti sijapenda hata kidogo kudhalilishwa kwa mwanangu ” mama mzazi wa marehemu

Akizungumzia mgogoro huo baba zazi wa marehemu amesema yeye alimwambia mkewe kuwa asubiri akazungumze na wenzake ila mkewe aliamua kuzika bila kumshirikisha baba

” mimi sikubali mwanangu azikwe kwa mama ake kwasababu mama ake ndugu zake wote wakiristo na mimi mwanangu muislam itakuwaje wamzike ” baba mzazi wa marehemu

” Mimi nimekwenda kwa sheha kuchukua barua pia polisi kuchukua RB na ndipo nikaenda kuchukua maiti ya mwanangu nikabeba mkeka shuka na kanga ili nikamzike mwanangu Matemwe ” baba mzaziwa marehemu

Chanzo: zanzibar24.co.tz