Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lupaso wasimulia alivyowagusa bila kubagua

Ff888cb4255892ae31808600721c33eb Lupaso wasimulia alivyowagusa bila kubagua

Tue, 28 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAISLAMU katika Kijiji cha Lupaso, wilayani Masasi, mkoani Mtwara na wa wilayani Masasi wamesema watamuenzi daima Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kwa kuwa bila kujali yeye ni Mkristo, aliwajengea misikiti miwili, mmoja kijijini na mwingine wa wilayani alichangia ujenzi wake.

Walisema watamkumbuka daima kwa kuwa hakuwa mbaguzi wa dini yoyote hatua iliyowaongezea umoja, mshikamano na upendo wananchi wa kijiji hicho kuishi kama ndugu.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Wilaya ya Masasi na rafiki wa karibu wa Mkapa, Alhaji Masoud Rajabu, alisema Rais Mkapa aliwajengea msikiti mzuri kijijini Lupaso na kama hiyo haikutosha, alishiriki ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Masasi wenye ghorofa mbili.

“Alikuwa rafiki kwangu na mtu asiye na ubaguzi wa dini yoyote. Ametujengea msikiti ambao hatukutarajia kuupata hapa Lupaso. Lakini pia alitoa mifuko ya saruji mingi kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa wilayani Masasi wa ghorofa mbili. Tutamkumbuka daima mzee wetu Mkapa,”alisema Rajabu.

Msemaji wa Msikiti wa Lupaso na mwanakijiji Mohamed Kitambi, alisema Mkapa aliwajengea msikiti huo muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa Rais.

Kitambi alisema kifo cha Rais Mstaafu Mkapa kwao ni pigo kubwa kwani wakati wa uhai wake aliwaunganisha wanakijiji bila kujali imani zao na kwa hakika taa ya Lupaso imezimika na wanakijiji wamekumbwa na mshituko mkubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz