Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukuvi awasili kutatua mgogoro wa ardhi wa miaka 42

65951 Pic+lukuvii

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi amefika eneo la Sinoni jijini Arusha kusikiliza mgogoro wa ardhi unaomuhusu, Nasi Muruo (98) uliodumu kwa miaka 42.

Mjane huyu licha ya kushinda kesi ya ardhi  tangu mwaka 1979 hajakabidhiwa eneo lake ambalo sasa kuna makazi ya kaya zaidi ya 50.

Lukuvi amewasili eneo hilo leo Jumatatu Julai 8, 2019 saa 5 asubuhi akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro.

Kikao baina ya Lukuvi na wakazi wa eneo hilo kitafanyika  uwanja wa shule ya msingi Sinoni.

Hivi sasa kikao cha ndani cha viongozi kinaendelea na baadaye utafanyika mkutano wa wazi.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz