Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukuvi amaliza utata wa viwanja Kijitonyama

2ad9a7960ec746c7120648adb722b30a Lukuvi amaliza utata wa viwanja Kijitonyama

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemaliza utata uliojitokeza mtaa wa Nzasa kata ya Kijitonyama katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam baina ya baadhi ya wakazi wa mtaa huo na mmiliki wa viwanja namba 296 na 297 vya Dk Khalifa Musa Msami kuhusiana na umiliki pamoja na mipaka ya eneo hilo.

Lukuvi amefika eneo hilo lililopo barabara ya Segera baada ya kupokea malalamiko kuhusiana na matumizi pamoja na mipaka ya eneo hilo ambapo alibaini ukiukwaji wa mipaka ya maeneo hayo huku baadhi ya wamiliki katika nyumba za mtaa huo wakiongeza ukubwa wa maeneo yao na kuingia sehemu ya barabarani kwa mita nne na wengine wakiziba mifereji ya maji taka.

Kufuatia hali hiyo, Lukuvi aliagiza ofisi ya ardhi Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na idara ya ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha inafufua mipaka ya maeneo hayo haraka ili kubaini wamiliki waliojiongezea maeneo kinyume na sheria.

“Uamuzi wangu baada ya kubaini ukiukwaji, timu ya wilaya na mkoa ije ifufue mipaka bila kubomoa nyumba na mjue ni kosa kujiongezea eneo. Ukimilikishwa jenga kwa mpango wa serikali siyo kujiamulia na heshimu mipaka ya serikali ” alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, timu kutoka ofisi hizo mbili itakapoenda kufufua mipaka katika eneo hilo itamuonesha kila mmiliiki eneo lake ambapo alisisitiza kuwa, baada ya kukamilika kazi hiyo kila mmiliki wa ardhi atatakiwa kubaki eneo lake kulingana na ukubwa wa kiwanja chake na maeneo ya barabara pamoja na njia za maji taka yaachwe wazi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz