Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukuvi: Halmashauri punguzeni urasimu

065903a7e55b83754e583fc3c06ef57d Lukuvi: Halmashauri punguzeni urasimu

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amezitaka halmashauri zote nchini kupunguza urasimu katika umilikishaji ardhi kwa sababu wao ndio wasimamizi wa ardhi yote nchini.

Waziri Lukuvi ametoa rai hiyo leo mkoani Iringa katika hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo na kuongeza kuwa mwekezaji yoyote awe wa kutoka ndani au nje ya nchi cha kwanza anachozingatia ni uwepo wa ardhi.

Akizungumzia Mwongozo huo, Lukuvi ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa kuandaa mwongozo huo ambao amesema ni nyaraka ya kwanza yenye taarifa zote za msingi kuwahi kuandaliwa katika ngazi ya mkoa.

Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani lililopo mkoani Iringa, amesema Wizara Ardhi ambapo sasa wameanzisha ofisi mkoani humo, hivyo wananchi na wawekezaji hawatahiji tena kwenda mkoani Mbeya kama ilivyokuwa awali.

Aidha amewataka wadau mbali mbali kushirikiana kutekeleza mwongozo huo, huku akitilia mkazo kuwa kuandika ni jambo moja na kutekeleza ni jambo lingine.

Chanzo: habarileo.co.tz