Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lucy: Nina mimba ya marehemu Bryan

Lucy  WA0004 Lucy: Nina mimba ya marehemu Bryan

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Arusha, Lucy Manyika amemuomba DC wa Arusha kusitisha kutoa fedha za rambirambi Tsh. milioni 5 zilitolewa na Rais wa Tanzania Dkt Samia Hassan kama mkono wa pole kwa Famiia ya Bryan Semunike Kijana aliyefariki kwenye ajali ya gari ya Shule ya Ghat Memorial wakati akiwaokoa Wanafunzi ambao gari yao ilisombwa na maji na kusababisha vifo ya Wanafunzi nane.

Mama huyo amesema Ndugu wa marehemu walimtenga tangu awali na kumzuia kushiriki masuala ya msiba ikiwemo kuweka mashada kwenye kaburi la Mchumba wake ilihali akiwa na ujauzito wa miezi mitatu wa Bryan.

"Nimeishi naye kwa mwaka mmoja tulikuwa kwenye process za kufunga ndoa, rambirambi zote zihusishwi na chochote Bryan alikuwa na miaka 35 Mimi nina 40 Ndugu zake wameshindwa kuelewa.

"Wifi yangu anasema Bryan alikuwa na Mke mwingine, naomba hizo fedha zirudi kwa Mkuu wa Wilaya tuitwe ili tujue Mke halali ni nani?"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live