Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori lililopata ajali Ruvu laondolewa barabarani, magari yaendelea na safari

71485 Ajali+pic

Thu, 15 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Abiria waliokuwa wamekwama katika eneo la Ruvu mkoani Pwani nchini Tanzania wameendelea na safari baada ya lori lililokuwa limepata ajali na kuziba barabara kuondolea.

Lori hilo ambalo lilipata ajali leo asubuhi Alhamisi Agosti 15,2019 na kuziba barabara Kuu ya Morogoro katika eneo la Ruvu lilisababisha abiria kukwama kuendelea na safari kwa saa mbili.

Hakukuwa na magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda uelekeo wa Morogoro au yanayotoka Morogoro kuelekea Dar es Salaam yaliyokuwa yanapita.

Awali, majira ya saa mbili asubuhi Mwananchi lililokuwapo eneo hilo lilishuhudia foleni kubwa ya magari mbalimbali ya abiria, madogo na ya mzigo.

Ajali hiyo haikusababisha madhara yoyote na baada ya lori hilo kutolewa eneo hilo, magari yaliendelea na safari.

Chanzo: mwananchi.co.tz