Dodoma. Mamia ya abiria na watumiaji wa barabara ya Dodoma- Singida nchini Tanzania wamekwama eneo la Salanda baada ya lori la mizigo kuziba barabara hiyo.
Lori hilo lilishindwa kupanda mlima Salanda na kuanza kurudi nyuma na kusimama katikati ya barabara hali iliyosababisha magari kushindwa kupita.
Hali hiyo imesababisha abiria waliokuwa wakienda mikoa mbalimbali kwa kutumia barabara hiyo pamoja na malori ya mizigo kukwama kuanzia saa 11 jioni leo Jumatano Oktoba 23, 2019.
Hadi saa 12:00 lori hilo lilikuwa halijaondolewa katika barabara hiyo.
Baadhi ya magari yanayotoka Singida kwenda Dodoma yalichepuka pembeni ya barabara hiyo na kupita katika shimo huku yanayotokea Dodoma kwenda Singida yakilazimika kusubiri hadi lori hilo litakapotolewa.
Mmoja wa abiria anayetoka Kahama mkoani Shinyanga kwenda Morogoro, Mussa Msafiri ameiomba Serikali kuwasaidia ili kuliondoa gari hilo.
Pia Soma
- Profesa Lipumba alilia Mapapala
- Mkuu wa JKT ataja siri ya kuteuliwa na Magufuli
- Sababu wakurugenzi mgodi wa Nyamahuna kukamatwa hizi hapa