Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori latumbukia mtoni, mmoja afariki Dunia

Lori Mroni Ajalii (33).jpeg Lori latumbukia mtoni, mmoja afariki Dunia

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya gari alilopanda kutumbukia katika Mto Lukuledi uliopo eneo la Mbecha, mkoani Lindi.

Akizungumza nasi jana Jumatano, January 17, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Lindi (RC), Zainabu Telack amesema lori hilo aina ya Howo likiendeshwa na Jafari Magumba, mkazi wa Kitangili, Shinyanga, lilitumbukia mtoni baada ya daraja kukatika.

Daraja hilo lipo katika eneo la Mbecha Barabara ya Mbecha -Ndanda kata ya Nanganga Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Telack amemtaja marehemu ni Debora Lutubija (28), mfanyabiashara na mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.

"Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani kwetu ndio zimesababisha kutokea kwa ajali hii kutokana na kukatika kwa daraja hili," amesema.

"Hii barabara ni ya changalawe kwa hiyo mvua ikinyesha udongo ukishaloana unasababisha kubaki na unyevunyevu ndio sababu ya kukatika kwa daraja hili," amesema mkuu huyo wa mkoa

Telack amesema mwili wa Deborah umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha afya Luchelegwa.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema dereva alikuwa anakwepa daraja la Ruangwa -Nanganga ambalo limejaa maji, “sasa dereva akaona bora apitie barabara hii ya Mbecha-Ndanda, mimi niombe Serikali kujitahidi kulijenga hili daraja kwa haraka."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live