Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori lapata ajali Ruvu, magari yakwama

71425 Ajali+pic

Thu, 15 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Abiria wanaotumia barabara Kuu ya Morogoro wamekwama kwa zaidi ya saa moja katika Eneo la Ruvu mkoani Pwani baada ya lori kupata ajali na kuziba barabara.

Kutokana na ajali hiyo iliyotokea leo Alhamisi Agosti 15,2019 hakuna gari linalopita eneo hilo iwe kwenda uelekeo wa Dar es Salaam au Morogoro na foleni ya magari ni kubwa kila upande.

Baada ya abiria wamediriki kushuka katika magari yao wakisubiri gari hilo kuondolewa ili kuwawezesha kuendelea na safari zao.

Akizungumza na Mwananchi kwa Simu Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema atafutwe RTO ili kupata taarifa.

"Mpigie RTO (Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani) atakupa taarifa", amesema kamanda Nyigesa

Alipopigiwa simu Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani kuulizwa sababu ya magari kukwama kwa muda mrefu alisema kuna ajali ya lori ambayo imesababisha kuziba barabara

Pia Soma

"Kiufupi kuna lori moja limepata ajali, tupo barabarani tunalikwamua ili magari yaendelee kupita" amesema RTO ambaye yupo kwenye eneo la tukio.

Amesema hakuna madhara kwa binadamu na wanajitahidi kuliondoa lori hilo.

 "Hakuna madhara kwa binadamu ni ajali ya kawaida" amesema RTO

Baadhi ya abiria wamesema kuwa wanahofu kuwa madereva watakwenda mwendo kasi ili kufidia muda waliokaa

"Hapa lori likishaondolewa mabasi yatakimbizana ili kufidia muda waliopoteza" amesema mmoja wa abiria anayesafiri kwenda  mkoa wa Mbeya

Dereva wa basi linalofanya safari za Dar es Salaam- Tunduma, Adam Iddi amesema "Hatuwezi kukimbia sana maana siku hizi tochi zimejaa kila sehemu ya barabarani.

 

Endelea  kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz