Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori lagonga daladala 3, lajeruhi watu 9

ARUSHAA 44 Lori lagonga daladala 3, lajeruhi watu 9

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: EATV

Watu 9 wamejeruhiwa usiku wa kuamkia leo Septemba 8, 2022, kwenye ajali iliyotokea katika eneo la Sakina jijini Arusha, baada ya lori lililokuwa limebeba shehena ya mahindi likitokea Arusha kuelekea Namanga kupoteza mwelekeo na kuzigonga daladala tatu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kusema kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini sababu ya lori hilo kupoteza mwelekeo na kusababisha maafa hayo.

Aidha Kama Masejo amesema kuwa, majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru, mkoani humo.  

Chanzo: EATV