Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori lafeli breki lagonga magari manne, mmoja afariki (+video)

Screen Shot 2020 07 22 At 2.21.23 AM 660x400.png Lori lafeli breki lagonga magari manne, mmoja afariki (+video)

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari la mizigo aina ya lori kufeli breki katika mteremko mkali wa Mlima Iwambi Jijini Mbeya na kisha kugonga magari mengine manne pamoja na bajaji.

AyoTV  imefika eneo la mteremko wa Mlima Iwambi na kushuhudia magari hayo ambayo yamepata ajali na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Sebastian Mbuta anasema chanzo cha ajali hiyo kimesababishwa na lori lililokuwa limebeba mbolea, mifumo yake ya breki kushindwa kufanya kazi na kugonga magari mengine.

“Lilifeli breki likagonga magari manne na bajaji, madereva zingatieni sheria za barabarani tuzuie ajali, nasisitiza watuamiaji wote wa barabara watii maelezo tunayowapa mara kwa mara” Kaimu Kamanda Mbeya

Chanzo: millardayo.com