Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori la mafuta laanguka Tanga, wananchi wachota mafuta

Operanews1671167747199 Lori la mafuta laanguka Tanga, wananchi wachota mafuta

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lori lililobeba shehena ya Mafuta ya Petroli limepata ajali na kuanguka katika eneo la segera Wilayani Handeni mkoani Tanga

Baadhi ya wakazi wa Segera walijitokeza na kuanza kuchota mafuta, hata hivyo muda mfupi baadaye polisi wamefika eneo hilo na kuwatawanya wananchi hao na hivyo kuepusha ajali ambayo ingetokea endapo moto ungewaka katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bi. Siriel Mchembe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Handeni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo

"Nalipongeza Jeshi la Polisi Handeni kwa kufanikiwa kudhibiti wananchi waliokuwa wanachota mafuta kwenye Gari la mafuta ya petrol lililopata ajali Segera. Hakika Mungu awabariki, wananchi chondechonde tusirudie tenaaaaaa!" - DC

Chanzo: www.tanzaniaweb.live