Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori la mafuta laanguka Kagera, waliochota mafuta wakamatwa

73057 Pic+lori

Tue, 27 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati machungu ya vifo zaidi ya 100 vilivyotokea na ajali ya lori la mafuta ya petroli yakiwa hayajasahaulika, Polisi mkoani Kagera nchini Tanzania linawashikiliwa watu wanane waliochota mafuta katika ajali ya lori mkoani humo huku wale waliokimbia wakiendelea kuwakwa.

Lori hilo la kampuni ya Lake Oil limepinduka leo Jumatatu Agosti 26, 2019 katika eneo la Rusumo wilayani Ngara ambalo lilikuwa linatoka nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam, Tanzania.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi ambaye alifika eneo la tukio amesema polisi waliokuwa katika kituo cha Benako waliwahi eneo la tukio ili kuhakikisha hayajitokezi maafa kama yaliyotokea mkoani Morogoro wiki kadhaa ziliopita.

Amesema jeshi hilo limekamata lita 300 za dizeli zilizokuwa zimechotwa.

“Tulitegemea wananchi kuwa wepesi wa kutii na kufuata maelekezo ya viongozi lakini pia sheria haiwaruhusu kwakuwa kuchota mafuta ni kitendo cha wizi,” amesema Malimi.

Aidha katika ajari hiyo dereva wa lori lililopinduka Juma Msafiri amepoteza maisha.

Pia Soma

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni siku 47 tangu ajali ya lori lililokuwa limebeba  shehena ya mafuta ya petroli lilianguka kisha kulipuka moto eneo la Msamvu mkoani Morogoro ambapo hadi leo Jumatatu vifo vimefikia 102.

Pamoja na vifo hivyo, majeruhi 13 wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dar es Salaam na 16 wapo Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Chanzo: mwananchi.co.tz