Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leseni 439 za uchimbaji wa madini zatelekezwa Simiyu

Siimiyu Pic Data Leseni 439 za uchimbaji wa madini zatelekezwa Simiyu

Mon, 12 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Leseni 439 za uchimbaji wa madini mkoani Simiyu zimetelekezwa na waombaji waliofanya maombi kwa njia ya mtandao baada ya kushindwa kukamilisha ufuatiliaji na kulipia ada.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika leo Septemba 11, 2022 kaimu ofisa madini mkazi mkoa wa Simiyu, Amini Msuya amesema jumla ya maombi 1,351 yalipokelewa na leseni 89 zimechakatwa na kutolewa kwa wadau.

"Changamoto kubwa kwa sasa ni wadau kufanya maombi mengi lakini hawafanyi ufuatiliaji wa hatua zinazofuata mpaka kuchukua leseni ikihusisha kulipa ada mbali mbali," amesema Msuya.

Uendeshaji wa shughuli za madini mkoani Simiyu unahusisha uwepo wa migodi ya wachimbaji wadogo 15, leseni hai za uchimbaji wa madini 256, mialo zaidi ya 300, mitambo 23 ya uchenjuaji udongo (VAT) na mitambo 5 ya uchenjuaji kaboni (Elutions).

Msuya yanayopatikana katika wilaya za Meatu, Itilima, Busega, Bariadi na Maswa ni metali (dhahabu, shaba na nikeli), madini ya vito (amethyst), madini ya viwandani (chokaa na chumvi) na madini ujenzi (mawe, mchango, moramu na kokoto).

Baadhi ya wachimbaji wadogo katika migodi ya Gasuma na Halawa wamebainisha changamoto walizonazo katika maeneo yao ya kazi ikiwamo kukosa huduma za nishati ya umeme hali ambayo wameitaja kama ni kuwadidimiza wachimbaji wadogo.

Advertisement Wamesema kucheleweshwa kwa huduma ya umeme katika maeneo ya mgodini inafanya shughuli za uchimbaji kuwa za gharama kubwa kwani inawalazimu kutumia mafuta kama nishati mbadala ambayo pia bei yake ipo juu.

"Kwa kutambua umuhimu wa uchangiaji wa mapato kutoka sekta ya madini serikali ingetupa kipaumbele tupate nishati ya umeme ili uwekezaji mkubwa ufanyike kwa gharama ndogo na hiyo utaongeza ukusanyaji wa mapato mara dufu" amesema Angelika Paul mchimbaji mdogo katika mgodi wa Gasuma.

Wadau wa madini mkoa wa Simiyu walipewa lengo la kukusanya Sh3 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022 lengo lililotimia hadi kufikia Desemba 2021, hivyo lengo la mwaka likaongezeka na kufikia Sh6 bilioni ambapo kufikia Juni 2022 walifanikiwa kukusanya Sh5.8 bilioni sawa na asilimia 97 ya lengo lililoongezwa.

Chanzo: Mwananchi