Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema atoa neno la Matumaini akiomboleza kifo cha Nisher

GBNcGLTXoAAygE .jpeg Lema atoa neno la Matumaini akiomboleza kifo cha Nisher

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, ametoa neno la matumaini kufuatia kifo cha mmoja wa watayarishaji maarufu wa video za muziki nchini, Nick Davie maarufu kama Nisher.

Katika akaunti yake kwenye mtandao wa X, Lema ameandika: “Maandiko kutoka katika Biblia yanatoa matumaini kwa watu wenye imani ya Kikristo kuwa kuishi ni Kristo na kufa ni faida. Hivyo kifo kwa Mkristo si tishio lolote bali ni njia ya kuanza maisha mapya ya milele.”

Lema ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini ametoa pole akisema: “Naamini Nisher atakuwa alikuwa ni mcha Mungu mzuri. Hata hivyo, ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na rafiki kwa sababu sasa watamkosa ndugu yao katika ulimwengu huu ambao ni wa muda sana kwa kila mmoja wetu. Pole sana familia yote ya GeorDavie."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live