Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Latra yawakomalia wanaopandisha nauli mabasi ya mikoani

89494 COSTAPIC Latra yawakomalia wanaopandisha nauli mabasi ya mikoani

Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema inapambana na wanaopandisha nauli za mabasi kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali nchini katika kipindi cha  kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Desemba 21, 2019  ofisa leseni wa mamlaka hiyo, Leo Ngowi amesema wameanza kufanya ukaguzi, ikiwa ni pamoja na kuwakamata mawakala wanaotoza nauli kubwa.

"Tumeanza kufanya ukaguzi tangu jana na kubaini mabasi yanayotoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kahama nauli zimeanza kupanda kiholela. Tumeshachukua hatua na wapo waliotozwa faini,” amesema Ngowi.

Kuhusu uhaba wa mabasi amesema umetokana na abiria kuongezeka, hasa wa mikoa ya Kaskazini.

“Mikoa yenye idadi kubwa ya abiria ni Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro na Dodoma. Katika kuhakikisha hali inakuwa shwari tumeongeza mabasi kwa kutoa leseni za magari madogo yenye uwezo wa kupakia abiria 40,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz