Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lami Tabora-Kigoma kukamilika 2023

Lami Barabaraaaa Lami Tabora-Kigoma kukamilika 2023

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewaahidi wakazi wa Mikoa ya Tabora na Kigoma kuunganishwa mikoa hiyo kwa barabara za lami ifikapo mwakani 2023.

Akizungumza kwa nyakati tofauti mkoani Kigoma na Tabora, wakati alipokagua miradi iliyobakia kuunganishwa mikoa hiyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza (km 51.1) na Kazilambwa - Chagu (km 36) kwa kiwango cha lami ni azma ya serikali ya kuunganisha barabara zote za mikoa na kuchochea shughuli za kibiashara.

“Serikali inayoongozwa na Mama Samia, inaendeleza Sera ya Ujenzi kwa kuhakikisha mikoa na wilaya zinaunganishwa kwa njia ya barabara bora, sambamba na miradi mingine ya uchukuzi ikiimarishwa, ili kumpa uhuru mwananchi achague usafiri atakaouweza", amefafanua Waziri Mbarawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live