Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LIVE: Mamia wajitokeza kilele mbio za Mwenge wa Uhuru

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Mamia ya watu wamejitokeza katika uwanja wa mpira wa Ilulu mjini Lindi katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru yanayofanyika sambamba na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ni Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Viongozi mbalimbali wameshiriki maadhimisho hayo akiwemo makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan; makamu wa pili wa rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro.

Chanzo: mwananchi.co.tz