Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LATRA yaanzisha njia mpya 11 Dar

56e06f99841fab03ac1e5d8ce7a49e06 LATRA yaanzisha njia mpya 11 Dar

Sun, 17 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), imeanzisha njia mpya 11 zitakazohusisha daladala takribani 170 na kukaribisha wasafirishaji kuomba leseni kwenye njia hizo mpya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kupitia kitengo cha mawasiliano cha Latra, kuanzishwa kwa njia hizo mpya kunalenga kufikisha huduma karibu na wananchi kwa mabasi yatakayokidhi vigezo.

Taarifa hiyo ilitaja njia hizo mpya kuwa ni kutoka Kigamboni kwenda Temeke kupitia Darajani, Uhasibu na Kilwa ambako jumla ya daladala 20 zinahitajika na kutoka Magole kwenda Machinga Complex kupitia barabara ya Nyerere ambako daladala 15 zinahitajika.

Njia nyingine mpya ni kutoka Magole kwenda Mnazi Mmoja kupitia barabara ya Uhuru (daladala 15), Magole kwenda Mnazi Mmoja kupitia barabara ya Nyerere (daladala 15) na Msingwa Shule kwenda Kawe kupitia barabara ya Morogoro, Sam Nujoma, Goba (mzunguko) daladala 10.

Aidha njia nyingine kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Msingwa Shule kwenda Makumbusho kupitia barabara ya Morogoro, Sam Nujoma, Goba (mzunguko) daladala 10.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo njia nyingine mpya ni Buyuni Sokoni kwenda Simu 2000 kupitia barabara ya Nyerere na Mandela daladala 20 zinahitajika, Buyuni Sokoni kwenda Kivukoni kupitia barabara ya Nyerere daladala 20 na Mnazi Mmoja kwenda Buza kupitia barabara ya usalama, Sudan na Majaribio daladala 20.

Njia nyingine ni Stesheni kwenda Buza kupitia barabara ya Kilwa na Majaribio daladala mpya tu 10 na Gerezani kwenda Buza kupitia Usalama, Sudan na Majaribio daladala mpya tu 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live