Mon, 25 Mar 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeeleza kutoridhishwa na kiwango cha utendaji kazi kinachofanywa na watendaji wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa LAAC Halima Mdee mara baada ya kupokea taarifa na kutembelea mradi wa Shule ya Sekondari ya Chatuu na hospitali ya wilaya ambapo yote kwa pamoja inaonesha kuwepo kwa viashiria vya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Katika kipindi cha miaka mitatu wilaya ya Muheza imepokea shilingi Billioni 91.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live