Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kura ya siri ilipigwa kuwabaini wanafunzi wanaodaiwa kuchoma moto mabweni

78400 Chalamila+pic

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chunya. Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Maryprisca Mahundi amesema ilipigwa kura ya siri kuwabaini wanafunzi 19 wa shule ya Sekondari Kiwanja mkoani Mbeya wanaodaiwa kuhusika na tukio la mabweni mawili ya shule hiyo kuteketea kwa moto.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila  aliyefika katika shule hiyo na kuwacharaza viboko wanafunzi 14 kati ya 19  wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo.

Wanafunzi watano kati ya 19 wanashikiliwa na polisi baada ya uchunguzi uliofanyika kuwahusisha moja kwa moja na tukio hilo huku wengine 14 wakiruhusiwa kuendelea na masomo.

Mabweni hayo yaliungua Septemba 30, 2019 saa 2 usiku,  chache baada ya kufanyika msako na wanafunzi hao kukutwa na simu 26 za mkononi jambo ambalo Mkuu wa shule hiyo, Elly Mnyarape amesema ni kinyume cha sheria za shule.

Maryprisca amesema baada ya kufika shuleni hapo, walifanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuendesha kura za siri ambapo wanafunzi 19 walikamatwa na kufikishwa Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Amesema kuwa baada ya mahojiano ambayo yalifanywa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya ya Chunya, wanafunzi 14 walionekana hawahusiki na kurejeshwa shuleni na wenzao watano wanaendelea kushikiliwa na Polisi wakihusishwa na tukio hilo.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Baada ya kutoa maelezo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila aliagiza kengere kugongwa na wanafunzi wote wakakusanyika ili kumsikiliza na ndipo alipowachapa bakora.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz