Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kupata kibali cha ujenzi Kigamboni wiki mbili tu

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kuanzia sasa wananchi wanaohitaji kufanya shughuli za ujenzi katika Manispaa ya Kigamboni, watapata kibali ndani ya wiki mbili tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Agosti 11, 2018 na mkurugenzi wa manispaa hiyo, Steven Kapemba  alipokutana na wenyeviti wa Serikali za mitaa ya manispaa hiyo kuzungumzia shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kapemba amesema sambamba na hilo watoaji vibali hivyo watakuwa wakiwafuata wahusika katika maeneo yao badala ya mtu kufunga safari kwenda ofisini.

Amebainisha kwamba ana imani mpango huo utasaidia kuharakisha maendeleo kwa wakazi wa Kigamboni ambao wanataka kuwekeza katika miradi mbalimbali.

"Kwa sasa hatuoni haja watu kupanga foleni kwa ajili ya kuomba kibali ofisini wakati suala hilo linawezekana kuchukua muda mfupi,” amesema.

“Kama mhusika katimiza vigezo vyote, watendaji wetu wataweka utaratibu wa kutembelea maeneo kwa zamu katika utoaji vibali.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz