Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetilia mkazo sheria ya ardhi na upangaji miji ambayo inamtaka kila mkazi katika eneo lake anapotaka kufanya ukarabati wa nyumba yake, kupaka rangi ama kujenga uzio lazima awe na kibali kutoka halmashauri.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Machi 12, 2020 mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli amesema kibali hicho hakitolewi bure bali kinalipiwa, kwamba kuhusu kiasi inategemea na aina ya ukarabati unaofanya.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu mjadala ulioibuka katika mitandao ya kijamii kuhusu suala hilo, jinsi wengi waliochangia kuonekana kutoijua sheria hiyo.
“Ni kweli, mwananchi yoyote anayetaka kupaka rangi, kufanya marekebisho ama kujenga ukuta ni lazima apate kibali kutoka mamlaka ya upangaji miji ambayo ni halmashauri, huu ni utekelezaji wa sheria ambayo ipo muda mrefu,” amesema.
Amesema kuwa watu wamezoea kufanya kazi kwa mazoea bila usimamizi wa sheria, kwamba sheria hiyo kwa sasa inatekelezwa.
Mkazi wa Kinondoni, Clemence Malya anayeishi Mikocheni amesema hana uelewa kuhusu sheria hiyo na alishangaa kuitwa serikali za mitaa kwa madai kuwa ameweka uzio wa nyumba yake bila kuwa na kibali.
Pia Soma
- Tanzania yapongezwa kudhibiti dawa za kulevya
- Waziri Ikupa awafunda wanawake walemavu
- Tanzania kuadhimisha wiki ya maji bila wageni kutoka nje, corona yatajwa
- VIDEO: Mchungaji Msigwa atoka jela