Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kunenge awataka wakazi wa Kunduchi Mtongani kuhama

6eb0df58f29ab1bf596b633d449898e3.jpeg Kunenge awataka wakazi wa Kunduchi Mtongani kuhama

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge amewataka wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na Volcano ya tope kuhama eneo hilo ili wajikinge na maafa yanayoweza kutokea kwao.

Kunenge amesema hayo leo Novemba 30 wakati alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapo.

“Wahame eneo lile ni hatarishi, nimeona nyumba zimepasuka nyingine zimezama, bado tunafanya uchunguzi wa kitaalamu kujua changamoto ni nini lakini kwa sasa wahame eneo hilo” amesema Kunenge.

Aidha, Kunenge amesema viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali wameshapita eneo hilo na jitihada zinafanyika namna ya kuwasidia kwa kuwapa hifadhi waliopatwa na maafa hayo.

Chanzo: habarileo.co.tz