Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kunenge awapa bodaboda ahueni

E6b20c1403775608ddf2376422ab00e5 Kunenge awapa bodaboda ahueni

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema serikali imepanga kuzuia uhalifu ili kuwawezesha waendesha bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu ‘Bajaji’ kufanya kazi bila usumbufu.

Akizungumza mapema leo katika ufunguzi wa kikao cha namna bora ya kutumia mtandao ili kudhibiti uhalifu wa vyombo vya moto hususani Bodaboda na Bajaji, Kunenge amewaomba washiriki wa kikao hicho kutoa mapendekezo ya namna ya kuzuia uhalifu.

“Ninawaomba washiriki wa kikao hiki muhakikishe mnafanya uchambuzi wa kina na kutoa mapendekezo yenye tija ni namna gani tutazuia uhalifu wa vyombo hivi ulioshamiri siku za hivi karibuni kwa kutumia mtandao” amesema Kunenge

Chanzo: habarileo.co.tz