Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kunenge ataka RITA ihamasishe uandishi wa wosia

Ca8e6f9f3b83c7627d67139a7a92e833 Kunenge ataka RITA ihamasishe uandishi wa wosia

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetakiwa kuendelea kuhamisha wananchi kujitokeza kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya mirathi katika familia mmoja wa wanafamilia anapofariki dunia.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakary Kunenge aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo alipotembelea banda la wakala huyo katika maonesho ya Wiki ya Mahakama.

Alisema pamoja na majukumu ya kuwaelimisha na kuwahudumia wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo ya utoaji wa huduma za usajili wa vizazi, udhamini, ndoa na talaka RITA inapaswa kuweka mkazo katika kutoa elimu kuhusu wosia ili wananchi wengi waweze kujitokeza na kuandikisha.

Aidha aliwataka wananchi wote hususani wakazi wa jiji hilo la Dar ces Salaam, kujitokeza mbele ya ofisi za wakala huyo kwa ajili ya kuandika wosia, jambo litakalowasaidia kuepusha aina mbalimbali za migogoro inayojitokeza katika familia kipindi mmoja wa wanafamilia hao anapofariki.

Akitoa maelezo kuhusu huduma hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka RITA, Edna Kamara, alisema licha ya elimu ya mara kwa mara wanayoitoa kuhusu huduma ya uandikaji wosia na utunzaji, bado kumekuwa na msukumo mdogo kwani wameandikisha chini ya watu 800.

Chanzo: habarileo.co.tz