Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kunenge apokea Kontena na Magari ya Usafi wa Mazingira

7231b4691836a41323613370e3cd60d3 Kunenge apokea Kontena na Magari ya Usafi wa Mazingira

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge leo amepokea magari 20 na kontena 65 za kuhifadhi taka zenye thamani ya Shilingi bilioni 4.1 ambapo amewahimiza wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira.

MKUU Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge leo amepokea magari 20 na kontena 65 za kuhifadhi taka zenye thamani ya Shilingi bilioni 4.1 ambapo amewahimiza wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira. Akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu, amesema “ni hatua nzuri kwa Jiji la Dar es salaam. Ni matarajio yangu kuwa Viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Manispaa, Jiji wataongeza kasi ya kusimamia vyema shughuli za usafi katika maeneo yao. Aidha kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira katika mitaa yetu.”

Chanzo: www.habarileo.co.tz