Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kunenge aongoza wananchi Pwani kuchanja corona

Bb407c49c0f0ef964775f49944c34b33.jpeg Kunenge aongoza wananchi Pwani kuchanja corona

Sun, 1 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameongoza wananchi wa mkoa huo kuchanja chanjo ya kujikinga na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19, ambapo mkoa huo umepokea dozi 6,000 za chanjo hiyo.

Uzinduzi wa chanjo hiyo kwa mkoa wa Pwani ulifanyika kwenye Kituo cha Afya cha Mkoani, mjini Kibaha.

Kunenge aliongoza uchanjaji chanjo pamoja na Katibu Tawala wa mkoa huo, Mwanasha Tumbo na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.

Alisema yeye amechanja na viongozi wengine pamoja na wananchi na hakuna aliyepata tatizo lolote na kuwadhibitishia ambao hawa- jachanja kuwa haina madhara yoyote kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuzindulia chanjo hii kitaifa, ambapo hata yeye amechanja na hakuna shida yoyote iliyotokea na wataalamu wametuthibitisha kuwa ni chanjo salama,” alisema Kunenge.

Alisema chanjo hiyo imeshafika mkoani humo na wataweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila mwananchi anayetaka anaipata.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Gunini Kamba alisema wananchi wanapaswa kuamini chanjo hiyo kwani imefanyiwa utafiti na imeonekana haina tatizo lolote.

Alisema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuielimisha jamii juu ya chanjo hiyo na kuondokana na dhana kuwa siyo salama.

Alisema tayari wameshatenga maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya kutolea chanjo ambapo kila mwananchi atapata chanjo hiyo kwa hiyari yake.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri aliwataka wananchi kujitokeza mara utaratibu wa kuchanjwa utakapowekwa.

Alisema amechanja chanjo hiyo na anajisikia vizuri, hivyo wananchi wasiwe na hofu na chanjo hiyo na kujitokeza kwa wingi kuchanja.

Chanzo: www.habarileo.co.tz