Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumekucha! RC Chalamila aagiza mkandarasi awekwe ndani

Ui.png Kumekucha! RC Chalamila aagiza mkandarasi awekwe ndani

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: Dar24

Mkuu wa Mkoa Kagera, Albert Chalamila ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani mkandarasi wa kampuni ya Sure Civil and Building Contractor ltd, baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi ya shule ya sekondari ya wasichana iliyopo kata Kanoni.

Chalamila ambaye alifika kukagua mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 4 ambapo shilingi bilioni 3 kati ya hizo imeshatolewa, amesema hajaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo na kwamba hatua zaidi zitafuata.

“Mimi huwa sichezewagi kwenye kazi, OCD si yupo hapa sasa huyu bwana anatakiwa akalale ndani halafu taratibu na maelekezo mengine yatafuata sijaridhishwa kabisa na hii kazi.

Amesema, watu wote walioshika miradi kwenye mkoa wa Kagera wanatakiwa kuzingatia utaratibu na kwamba endapo watafanya kazi kwa mazoea basi wataumia.

Chanzo: Dar24