AGOSTI 10, 2023 ni miaka minne tangu kutokea kwa ajali ya moto ambayo kiini chake kilikuwa ni kupinduka kwa lori la mafuta na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na bado makovu ya ajali hiyo hayajapona mioyoni mwa waliopoteza wenza wao ,ndugu , watoto na jamaa zao.
Ajali hiyo ilitokea Agosti 10, 2019 majira ya saa mbili asubuhi, baada ya gari aina ya lori namba T 717 DDF lilikuwa na tela namba T 645 CAN lililokuwa limebeba mafuta ya petroli na dizeli kupinduka eneo la Maraha - Msamvu ,Manispaa ya Morogoro , barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyokuwa imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa lori la mafuta walifikia 100, wakiwemo wale waliofariki baadaye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili , Dar es Salaam.