Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe aliyepora maiti Tanga hajajinyongea mahabusu!

Qjali Coaster Tanga 33 Kumbe aliyepora maiti Tanga hajajinyongea mahabusu!

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba amesema mahabusu aliyeripotiwa kujinyonga alikuwa uraiani na sio mahabusu kama ilivyoelezwa awali.

Mtuhumiwa huto ni mmoja kati ya 14 waliokamatwa wakihusishwa na uporaji mali za abiria waliofariki na kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo aina ya Coaster na lori aina ya Fusso Februari 4, 2023.

"Hawa waliokuwa mahabusu sio mahabusu kwa sasa, tulivyowafikisha mahakamani walipata dhamana na walikuwa nje na hata hili tukio la kujinyonga halijatokea mahabusu limetokea uraiani"

"Siku ya kuripoti mahakamani Bw. Said Charles hakutokea mahakamani na mtoto wake ambaye alimuwekea dhamana kutomuona mahakamani na kuanza kumtafuta wakapata wasiwasi na kuanza kumtafuta"

"Jana wajukuu zake, ndugu na marafiki walifanikiwa kumuona huko shambani kwake akiwa amejinyonga kwenye mti kwa kutumia neti ya Mbu na baada ya hapo walitoa taarifa polisi na timu ya uchunguzi ndio ikaenda eneo la tukio" - Omary Mgumba RC Tanga.

Basi hilo lilikuwa likisafirisha msiba kutoka Dar es Salaam kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na ndipo lilipogongana na Fuso katika kijiji cha Magila wilayani Korogwe mkoani Tanga na kusababisha vifo vya watu 20 katika eneo hilo na wengine kufia hospitali.

Kufuatia ajali hiyo, baadhi ya watu waliodaiwa kupora mali katika eneo hilo walikamatwa. Amesema awali walikamatwa watuhumiwa 14, lakini watuhumiwa sita waliachiliwa baada ya kufanyika mchujo.

Mgumba amesema, mtuhumiwa aliyejinyonga ni ambaye wakati wa upekuzi uliofanywa na polisi nyumbani kwake kulikutwa na baadhi ya vitu zikiwamo simu, begi na nguo vikiwa na alama za damu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live