Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kulwa auawa na mamba akioga

Mamba Kulwa auawa na mamba akioga

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa kijiji cha Buzimbwe wilayani Bunda mkoani Mara, Kulwa Silas (46), amefariki dunia kwa kuliwa na mamba ziwani, wakati walipokwenda kuoga na mke wake.Mke wa marehemu Kulwa ambaye jina lake halijafahamika amesimulia ilivykuwa:-

“Aliniambia mke wangu najisiki kuoga nipeleke ziwani, na mimi nilikuwa na kazi ya kupepeta mahindi, nikamwambia basi twende nikupeleke mke wangu ndipo tukateremka tukafika nikachota maji mimi nikaogea pembeni, nilipomaliza kuoga na yeye alikuwa anamalizia, akachuchumaa kujimwagia maji, nilisikia ‘Paah’ nay eye akafanya ‘Ahhh’ ndo safari ya mume wangu ikaishia hapo”

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo amesema kuwa; “Tunaiomba serikali waweke mikakati ya kudhibiti hawa mamba, kwasababu hawa mamba sisi hatuna faida nazo, zinatuulia watu, mamba wenyewe ndo wanafugwa. Hawa watu wanaouawa ndo wanaohudumia familia zao, mamba hawawezi kuhudumia familia za hao watu wanaowachukua. Maji hayatoki mwezi mzima.”

Tukio hilo limetajwa kufikisha idadi ya watu sita ambao wameuawa na mamba kwa kipindi cha mwezi mmoja katika vijiji tofauti wilayani humo, hali ambayo imezua hofu na taharuki kwa wananchi wa vijiji vinavyozunguka Ziwa Victoria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live