Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kukosa chakula kwaathiri matokeo la 7, kidato cha 4

C778c7fc64912abf6ec062ac2affcb6c Kukosa chakula kwaathiri matokeo la 7, kidato cha 4

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

OFISA Elimu Mkoa wa Songwe, Juma Kaponda, amesema kukithiri kwa udumavu na ukosefu wa chakula cha mchana katika shule za awali, msingi na sekondari mkoani humo kunasababisha matokeo mabaya ya darasa la saba na kidato cha nne.

Alisema hayo katika kikao cha lishe cha mkoa kilichoshirikisha viongozi wote wa mkoa na halmashauri zote za mkoa wa Songwe kujadili namna ya kutathmini na kutatua udumavu kwa kuwa mkoa ni miongoni mwa mikoa mitano inayozalisha kwa wingi mazao ya chakula.

Alisema licha ya vyombo vya habari kuripoti mara kwa mara kuhusiana na udumavu takwimu za kitaifa zinaonyesha, mkoa wa Songwe una udumavu kwa asilimia 43, hali inayoathiri sekta ya elimu kwa kiasi kikubwa.

Alisema kukithiri udumavu kunasababisha ufundishaji watoto kuanzia ngazi ya awali, msingi na sekondari kutoelewa haraka Ikilinganishwa na watoto ambao hawana udumavu.

Kaponda alisema serikali imezitaka shule zote za kutwa kuanzia ngazi ya awali kutoa chakula cha mchana, lakini kwa mkoa wa Songwe bado ni shule chache za kutwa zinazotekeleza agizo hilo.

"Kwa mwaka jana watoto walioandikishwa kufanya mtihani walikuwa 20, 353, lakini waliofanya mtihani ni 19, 967 sawa na asilimia 98 ya waliosajiliwa, matokeo yalipotoka waliofaulu ni 15, 075 sawa na asilimia 75.51, katika ufaulu huo wanafunzi zaidi ya 14,000 sawa na silimia 81 walipata daraja la C.

Ofisa Lishe Mkoa wa Songwe, Mussa Mlemilwe, alisema udumavu mkoani humo unasababishwa kwa kiasi kikubwa na kutozingatia kanuni bora za mpangilio wa chakula kwa mtoto na aina ya vyakula anavyotakiwa kupewa tangu anazaliwa mpaka kufikisha miaka mitano.

Alisema sababu nyingine ni asilimia kubwa unyonyeshaji watoto kwa mkoa huo kutokuwa mzuri licha ya akina mama wengi kujifungulia katika zahanati na vituo vya afya.

Mganga Mkuu Mkoa wa Songwe, Hamad Nyembea, alisema udumavu ni suala la mtambuka, kwa kuwa huathiri mifumo mingi hasa elimu, uongozi na uchumi

Chanzo: habarileo.co.tz