Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kukosa chakula chanzo utoro Urambo

194a47e015655bcde43c86f94cabf8c8 Kukosa chakula chanzo utoro Urambo

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UKOSEFU chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Urambo mkoani Tabora umetajwa kuwa moja ya vyanzo vya utoro kwa wanafunzi; Imefahamika.

Mkuu wa Wilaya hiyo Angelina Kwingwa alisema wakati mwingine watoto wanaenda shuleni bila kupata chakula nyumbani hivyo kusababisha washindwe kuelewa darasani kwa sababu ya njaa.

Katika ziara yake kuzungumza na wananchi, Mkuu wa Wilaya hiyo alisema, njaa shuleni imekuwa ikisababisha wanafunzi kukata tamaa na kuamua kufanya vitu vinavyosababisha wawe watoro na kuingia katika vishawishi ili wapate chakula.

“Watoto wakati mwingine huwa tunawalaumu bure, wakati chanzo ni sisi wazazi kwa kuwa tunashindwa angalau kumchangia mtoto chakula akala shuleni; wakati mwingine watoto huondoka bila kula nyumbani na unakuta usiku pia hakula sasa ataelewaje darasani,” alisema Kwingwa.

Alisema, watoto wa kike wanakumbana na changamoto kubwa na wengine kujitumbukiza katika vishawishi na kufanya mambo yasiyofaa, ikiwa ni pamoja na kujitumbukiza katika uhusiano ya kimapenzi ili wapate fedha za chakula.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo wa Kata ya Mchikichini, Athumani Mwiniko, alisema waliweka utaratibu kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni katika Shule ya Msingi Umoja na Sekondari ya Chetu zilizopo katika kata hiyo kwa kuiagiza kamati za shule kukaa na wazazi wa wanafunzi na kukubaliana kuchangia.

Ofisa Utamaduni na Michezo wa Wilaya ya Urambo, Tito Lulandala alisema ipo tabia ya baadhi ya wazazi kugoma kuchangia chakula wakiamini mtoto kupatiwa chakula shuleni ni jukumu la serikali na shule.

“Kuna baadhi ya wazazi wanajua chakula ni jambo la shule ndio maana hata serikali za vijiji na kamati za shule zinapoitisha mikutano ili wachangie baadhi yao hugoma,” alisema Lulandala

Chanzo: habarileo.co.tz