Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kukatika umeme Mbeya hadi wiki tatu

Umeme Pic Ff Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema Serikali inaendelea kulifanyika kazi tatizo la kukati umeme mara kwa mara jijini humo akiahidi kuwa ndani ya wiki tatu tatizo hilo litaisha.

Hivi karibuni Jiji la Mbeya limekuwa na tatizo la kukatikakatika umeme na kusababisha shughuli kutofanyika kwa ufanisi.

Akizungumza kwenye kikao kilichowashirikisha wamiliki wa viwanda na taasisi mbalimbali, Homera amesema tatizo hilo lipo lakini Serikali inaendelea kulifanyia kazi.

Amesema wanatarajia ndani wiki mbili hadi tatu changamoto hiyo inaenda kuisha na kuwaomba wamiliki wa viwanda na wananchi kuvuta subra kwani Wizara na Serikali wanalifanyia kazi.

"Nielezee suala la umeme, umekuwa ukikatikakatika niwatoe hofu watu wa viwanda na wananchi kwamba Serikali na wizara tunalifanyia kazi na ndani ya wiki tatu tatizo litaisha" amesema Homera

Kwa upande wake Mahenge Cyprian amesema watendaji wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwani imekuwa ni changamoto kwa watu wenye viwanda kukwama kwenye shughuli zao.

"Lazima hawa watendaji nao wawe makini kutekeleza wajibu wao, niwaombe kulishughulikia haraka tuweze kufikia malengo" amesema Cyprian.

Chanzo: mwananchidigital