Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kopo la maji lasababisha vifo

Kopo La Majiii Kopo la maji lasababisha vifo

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wawili Jeplus Marco (3) na Martin Lameck (1) wamefariki baada ya kuzama kisimani wakiwa wanafuata kopo lililokuwa linaelea kisimani katika Mtaa wa Nyantorotoro B, Malmashauri ya Mji Geita.

Mwakilishi wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Emmanuel Ndosi amethibitisha kutokea tukio hilo jana jioni, huku akitoa rai kwa wananchi kuwalinda watoto hasa wanaoishi katika maeneo karibu na visima vya maji na mabwawa ili kuepuka matukio ya watoto kupoteza maisha.

Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Nyantorotoro, Khadija Mzee ameagiza kufunikwa visima, madimbwi pamoja na mashimo yote.

Wazazi wa watoto hao wamesema waliwaacha watoto nyumbani wakicheza wakati wakiwa wameenda shambani kulima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live