Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kongwa kutangaza mchango wake ukombozi nchi za Afrika

Vlcsnap 2023 07 10 10h49m45s694 1024x576 1.png Kongwa kutangaza mchango wake ukombozi nchi za Afrika

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini, imeandaa mbio za Marathon kwa lengo la kuutangaza mchango wa Wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla, katika ukombozi wa nchi za Afrika.

Hayo yamesemea hii leo November 16, 2023 na Mkuu wa Wilaya hiyo, Remidius Mwema wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya kuitangaza Wilaya hiyo kupitia mbio za Marathon, zitakazoanza November 25, 2023 Wilayani Kongwa, Dodoma.

Amesema, “kupitia mbio hizo Ofisi itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuyatambua maeneo ya kihistoria, kuyalinda, na kuyaendeleza ili kuenzi historia yataifa na kufanya sehemu ya utalii wa kihistoria katika maeneo ya urithi wa ukombozi yaliyopo Nchini.”

Aidha ameongeza kuwa, “Kongwa liberation Marathon imezingatia taratibu zote za marathon na kwamba zimegawanywa kwenye makundi ya Kilomita 5,Kilomita 10 na Kilometa 21, mgeni rasmi wa mbio hizo anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro.”

“Wilaya ya Kongwa imegusa ukombozi na historia ya harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini,Zimbabwe,Angola na Msumbiji na hivyo kuwa na nafasi ya kujitangaza kama sehemu ya vivutio vya utalii,” amesema.

Hata hivyo, amefafanua kuwa, “Serikali itashirikiana na nchi tulizozipa hifadhi wakati wa harakati za ukombozi kwa kukarabati majengo yaliyotumika na wapigania uhuru wa Afrika ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wao na kuitunza historia hiyo kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae.”

Remidius ameongezea kuwa, “kupitia Marathon Wilaya hiyo itatangaza fursa za Uwekezaji zilizopo ikiwemo Kilimo, Viwanda, Ranchi ya taifa, Soko la kimataifa la Mahindi Kibaigwa na Hoteli za kitalii kwani Kongwa ni lango la kuingia Makao Makuu ya nchi tunategemea kuwa sehemu ya kivutio cha utalii na uhifadhi wa historia, hivyo tumetenga eneo la Pandambili kwa ajili ya Uwekezaji wa viwanda.”

Chanzo: Dar24