Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kongamano la uwekezaji kufungua fursa mkoani Ruvuma

68839 Waziri+pic.png

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songea. Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Serikali ya Tanzania, Mhandisi Stella Manyanya amesema Maonyesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji Ruvuma, litaleta fursa nyingi za kibiashara na uchumi mkoani humo.

Waziri Manyanya ameyasema hayo Jumamosi Julai 27, 2019 mjini Songea, mkoani Ruvuma.

Amesema Mkoa wa Ruvuma umejaliwa kuwa na fursa nyingi na kwa muda mrefu, mkoa huo haujafanya tukio kama hilo,  lakini sasa kupitia kongamano hilo litawafungua  kuwafahamisha watu mbalimbali kuwa nini kinapatikana mkoani humo.

Amesema changamoto zinazowakabili wawekezaji wadogo ni pamoja na upatikanaji wa mitaji,  lakini kwa sasa Ruvuma umepata mkombozi hususan Benki ya NBC ambayo inatoa mikopo mikubwa na midogo kwa masharti nafuu kwa wananchi na wawekezaji.

 "Nawakaribisha sana wawekezaji na wadau wote ambao wana nia thabiti ya  kuja kuwekeza Ruvuma, mkoa huu una umeme wa kuridhisha hivi sasa unaoweza kukidhi,” amesema Naibu waziri huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Tawi la NBC Songea, Simon Ntwale amesema maonyesho hayo yamekuwa fursa nzuri kwa Benki ya  NBC kwa sababu wameweza kukutana na wadau mbalimbali watakaoweza kufungua fursa mbalimbali za kibiashara.

Pia Soma

Amesema benki ya NBC imepata faida ya kuingia mkataba na taasisi ya PASS, ambapo wanakwenda kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya kilimo na mkopaji anaweza kupata pembejeo za kilimo.

Ntwale pia amewatoa shaka wakulima wakubwa na wadogo pamoja na wachakataji na wawekezaji wadogo kujitokeza kwa wingi ili kupata mkopo endapo kampuni ya PASS  itakuwa imeadhinisha kwa mteja husika kupata mkopo huo.

 "Wawekezaji na wakulima wadogo msiogope kuitumia Benki ya NBC kwani ni benki yenu ambayo ipo tayari  kuwasaidia ili mtimize malengo yenu kwani wengi wamenufaika na mikopo hiyo hadi sasa wanafanya biashaza za mazao yao hadi nje ya nchi," alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa huo, Christina Mndeme alisema kutokana na kufunguka kwa miundombinu mbalimbali kama umeme na barabara, mkoa huo sasa umekuwa kivutio kwa wawekezaji nchini wa ndani na nje.

Chanzo: mwananchi.co.tz