Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Koboko wa maajabu auawa Tabora

 Koboko Black Mamba.jpeg Koboko wa maajabu auawa Tabora

Thu, 28 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Koboko ndiyo nyoka hatari kuliko nyoka wote hapa duniani na hii ni kwa sababu ya mkusanyiko wa sumu kali alionao, nyoka huyu ana aina mbili za sumu ambazo hufanya kazi kwa pamoja na endapo mtu atang’wata basi ndani ya dakika 3 hadi 10 mtu huyu akikosa matibabu hupoteza maisha.

Nyoka hawa huwa na maeneo maalumu ya kung’ata ambayo ni kichwani, shingoni au kifuani kwani mara nyingi hukaa juu ya mti, na ukiwakuta chini urefu wao ni futi 16 na akiwa na hasira husimama nusu mwili wake ambapo ni sawa na futi 8.

Wataalamu wanashauri jinsi ya kumuua ni kuchemsha chungu cha maji ya moto au uji kisha kujitwika kichwani na kupita maeneo ambao wanapatikana nyoka hawa, wakitaka kung’ata katika maeneo yao huishia kudumbukia ndani ya chungu hiko chenye kimiminika cha moto, hufa.

Lakini pia nyoka huyu unaambiwa anauwezo wa kutembea mwendo kasi mkubwa sana ambapo anaweza kukimbia 23km hadi 25km ndani ya saa moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live