Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kliniki ya ardhi yafika Ubungo

Jerry Silaa Awataka Wakuu Wa Mikoa Kutekeleza Maamuzi Baraza La Mawaziri Kliniki ya ardhi yafika Ubungo

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamishna na watumishi wa wizara ya ardhi wametakiwa kusimamia vyema zoezi la utoaji huduma kwa wananchi kupitia programu ya Kliniki ya Ardhi ambapo wananchi wanapatiwa huduma zote za umiliki wa hati na kutatuliwa changamoto zake.

Akizungumza na wananchi wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo, Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anamiliki hati ya ardhi yake.

Silaa amesema awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za kupata hati ya ardhi ndio sababu ya Serikali ikaona haja ya kuwafuata wananchi waliko ili kuwawezesha kupata hati hizo kwa urahisi bila urasimu kama awali.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam, Shukrani Kyando amesema zoezi hilo litadumu kwa siku 25 katika wilaya ya Ubungo na kuhimiza wananchi kujitokeza kupata hati za ardhi na kutatuliwa changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live