Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha Dangote chapewa siku 14 kuondoa migogoro

KYO Ed.jpeg MKUU wa Wilaya ya Mtwara Dustan Kyoba

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

MKUU wa Wilaya ya Mtwara Dustan Kyoba, ameuagiza uongozi wa Kiwanda cha kuzalisha simenti cha Dangote kilichopo mkoani humo kuhakikisha wanapatia ufumbuzi madai ya wakazi 17 wa kijiji cha Imekuwa wilayani humo juu ya mashamba yao kuathiriwa na vumbi la simenti inayozalishwa na kiwanda chao.

Amesema ufumbuzi huo unapaswa uwahusishe wananchi wanaodai mashamba yao kuathiriwa pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kuimarisha ujirani mwema baina ya kiwanda hicho na wakazi walio jirani.

Kyobya ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua uchimbaji wa kisima katika kijiji cha Imekuwa, uchimbaaji unaofadhiliwa na kiwanda cha Saruji cha Dangote ambapo mpaka kukamilika kwake itaghjarimu shilingi milioni 26.8.

"Nawaelekeza Dangote suala hili lipatiwe ufumbuzi ndani ya siku 14 na mniletee majibu kwangu kwa kuwa linawagusa wananchi moja kwa moja na lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi hawaathiriki na aina yeyote ya uwekezaji unaofanyika nchini" amesema Kyobya

Akizindua uchimbaji wa kisima cha maji Kyobya, amesema wananchi wanapaswa walinde mradi huo wa maji kwa wivu mkubwa kwa kuwa asilimia 75 ya shughuli za kiuchumi kwa mwanadamu zinategemea upatikanaji wa maji ya uhakika.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwaagiza mamlaka ya maji mkoa wa Mtwara kuhakikishaa miundombinu ya maji inafikishwa katika kijiji hicho kwa ajili ya kuwarahisishia maisha wakazi wake walio katika vitongoji vinne'

Meneja Mawasiliano wa Dangote Rachael Singo, akizungumzia maagizo hayo ya Mkuu wa Wilaya, amesema watashughulikia malalamiko ya wakazi hao 17 na kupata suluhu ya kudumu

Kuhusu uchimbaji kisima ameeleza kuwa wakazi wa kijiji cha Imekuwa watakabidhiwa kisima hicho katika muda wa wiki mbili kuanzia leo, huku akiahidi uchimbaji mwingine wa kisima katika kijiji cha jirani cha majengo kabla ya Disemba mwaka huu.

Awali mwenyekiti wa kijiji cha Imekuwa Juma Hussein alimueleza Mkuu wa wilaya kero mbali mbali za kijiji hicho ikiwemo wazee kutonufaika na huduma za bure za matibabu pamoja na wanaostahili kupata msaada wa Tasaf kutokupata kwa miaka mitatu sasa.

Chanzo: ippmedia.com