Hii imebainishwa leo Julai 22, 2023 na Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndungulile katika akaunti zake za Twitter na Instagram pale alipo andika: “Kivuko cha MV Kigamboni kimepata hitilafu. Matengenezo yanaendelea. Wenye magari mnashauriwa kutumia daraja la Nyerere. Matengenezo yanatarajia kukamilika saa 7 mchana. Aidha, nimejulishwa kuwa mfumo wa malipo umetengemaa.”
Hata hivyo mmoja wa watu wanaomfuatilia mbunge huyo katika akaunti yake ya Twitter, Gody Idabu, licha ya kushukuru kwa taarifa hiyo, amehoji ni mikakati ipi imewekwa ili kuondoka na taarifa hasi juu ya vivuko hivyo.
“Mheshimiwa, upo vizuri kwenye kutoa taarifa mapema ila ‘for how long’ (ni kwa muda gani) tutakuwa tunaendelea kupata taarifa ‘negative’ (hasi) tu, itakuwa vyema kama utaweza kutuambia miakakati gani inafanyika kuimarisha suala la vivuko, ili siku moja tukute hapa taarifa ‘positive’ (chanya) kuhusu vivuko na iwe kikomo cha hizi taarifa mabaya,” ameandika Idabu.