Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kituo cha Afya Murriet chafurika maji, huduma zasimama

OY9uzHsa.jpeg Kituo cha Afya Murriet chafurika maji, huduma zasimama

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zimesababisha Kituo cha Afya cha Murieti kujaa maji katika wodi za wagonjwa na maeneo ya kuhifadhi dawa na kusababisha huduma hiyo muhimu kusimamisishwa.

Maji yalianza kuingia katika Kituo hicho usiku wa kuamkia leo Novemba 15, 2023 kuzua adha kwa wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo ambayo imejengwa hivi karibuni.

Mariam Issa, mkazi wa eneo hilo amesema ameshindwa kufanya kupatiwa huduma kutokana na kituo kujaa maji na kutakiwa kisubiri hadi pale maji yatakapoondolewa.

"Wametuambia tusubiri maji yatolewe ndio huduma ziendelee, mimi nilikuja kwa ajili ya kliniki," amesema.

Kwa upande wake, Ramadhani Ally mkazi wa eneo la Kwa Mrombo Murieti amesema mvua zimekuwa na madhara makubwa katika Jiji la Arusha.

"Tunaomba hatua za dharura kusaidia kupunguza athari za mvua hasa kukarabati mifereji ya maji na barabara,"amesema Ally.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dk Maduhu Nindwa amekiri kituo hicho kujaa maji na amesema wameanza jitihada za kuyaondoa maji hayo.

"Jiji tayari limetoa gari la kuondoa maji na kuchimba mitaro (excavator) ili kuzuia maji zaidi kuingia katika kituo hicho,"amesema Dk Nindwa.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Hamsini amesema Jiji limeanza kukabiliana na athari za mvua katika sekta ya afya kwa kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya marekebisho ya miundombinu iliyoathirika.

"Tumetenga Sh200 milioni kukabiliana na athari za mvua na hili lililotokea kituo cha Afya Murieti tutapeleka Sh20 milioni kukarabati mfumo wa maji na kuondoa maji yaliyoingia ndani na yaliyotuama.

"Tumejiandaa kukabiliana na changamoto zote za mvua katika Jiji la Arusha,"amesema na kuongeza.

Mbali na maji hayo kuingia kituoni hapo pia mvua zimeharibu barabara ambayo inaelekea katika Kituo hicho cha afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live