Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisarawe waanzisha mpango kuinua masomo ya sayansi

Kisarawepic Data Kisarawe waanzisha mpango kuinua masomo ya sayansi

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wilaya ya Kisarawe kwa kushirikiana na Chuo cha City College Health kampasi ya Ilala wamezindua mpango wa miaka mitano wa kuinua masomo ya sayansi wilayani humo.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon 'Nikki wa Pili' amesema katika mpango huo wataanzisha na kuboresha shule za ujuzi na vipaji maalum na kwamba kupitia mpango huo pia watasomeshwa bure wanafunzi katika fani ya udaktari katika wilaya hiyo.

"Kwa hiyo makubaliano haya yatahusisha kuziongeza shule uwezo, tayari tumeajiri walimu wanne katika Shule ya Sekondari Kimani  kwa miaka mitano  ambapo mishahara italipwa na City College.”

"Pia vitabu 100 vya masomo ya sayansi vimenunuliwa katika shule hiyo pamoja na  kujenga maabara za Tehama. Natumia fursa hii kuwashukuru kwa kuamua kuisapoti Kisarawe katika masomo ya sayansi lengo kuu ni kuwa na Kisarawe yenye ujuzi," amesema Nikki wa Pili.

Naye mkurugenzi wa chuo hicho, Dk Shabani Mwamba amesema pamoja na hayo pia madaktari 500 watapiga kambi Kisarawe kupima na kutibu bure.

"Sisi kama wadau wa masuala ya sayansi, tukaona tuje kuisapoti Kisarawe kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ili kuanzisha na kuboresha shule ya ujuzi na vipaji maalum.”

Advertisement "Hii ni hatua ya mwanzo tu lakini tutaendelea kuisapoti Kisarawe katika mambo mbalimbali ili kuhakikisha inapiga hatua zaidi na tunawasaidia wanafunzi wetu kutoka hatua moja kwenda nyingine," amesema Dk Mwamba.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz