Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa chanjo ya Corona, wanafunzi watimua mbio wakiona magari

9a532e9e23e5aad7488e035b4f640735 Kisa chanjo ya Corona, wanafunzi watimua mbio wakiona magari

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANAFUNZI wilayani Geita wamekumbwa na hofu ya kukimbia madarasani kila waonapo gari shuleni wakihofia kuchomwa chanjo ya Corona.

Kufuatia hali hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Edith Mpinzile, amewaagiza wazazi, walimu na maafisa elimu kutoa elimu kwa wanafunzi kuwa chanjo ya Corona ni hiari na haitolewi kwao kufuatia kukithiri vitendo vya wanafunzi kukimbia madarasani kila waonapo gari wakihofia kuchomwa chanjo hiyo.

Maagizo hayo ameyatoa wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo wilayani humo uliofanyika kwenye kituo cha afya Katoro, ambapo amesisitiza kwamba elimu itolewe ili kuondoa hofu kwa watoto na watambue kwamba magari yanayofika mashuleni mwao yanaenda kwa shughuli maalum za ufuatiliaji wa elimu.

Baadhi ya wazazi waliofika kituoni hapo kwa ajili ya kupata chanjo wameelezea sababu zinazopelekea watoto kukimbia waonapo magari mashuleni mwao ni upotoshaji mkubwa ambao umefanywa na baadhi ya wazazi wao kuwa chanjo inagandisha damu zao kitendo ambacho kimewajengea watoto hao kuwa na hofu.

Chanjo ya corona inayotolewa sasa ya kampuni ya Johnson & Johnson hairuhusiwi kuchanjwa mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18 na zoezi lake linafanyika kwa hiari.

Chanzo: www.habarileo.co.tz