Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi mbio za Mwenge awapa somo watumishi wa Serikali

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msalala. Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,  Mzee Mkongea Ali amewataka watumishi wa Serikali kutotekeleza miradi ya maendeleo kwa mazoea na kuwataka kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 8 wakati wa makabidhiano ya Mwenge kutoka mkoa wa Geita kwenda mkoa wa Shinyanga.

Amesema miradi ambayo haikupitiwa au kuzinduliwa na mbio za Mwenge imetokana na watumishi kutofuata sheria, taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Mwenge kwa mkuu kwa mkoa wa  Shinyanga, mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya Sh12 bilioni iliyokataliwa na mbio za Mwenge inachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kujiridhisha kama inalingana na thamani ya fedha zilizotumika.

Gabriel amesema Mwenge wa Uhuru mkoani Geita ulilenga kuzindua, kufungua na kutembelea miradi 70 yenye ya Sh32.4bilioni lakini kutokana na kasoro zilizojitokeza umekagua miradi 65 yenye thamani ya Sh20.3 bilioni.

Miradi iliyokataliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge ni ya maji katika halmashauri za Bukombe, Geita na mradi wa daraja katika halmashauri ya Nyang’wale.



Chanzo: mwananchi.co.tz