Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi CCM wilayani Muleba akutwa amekufa

96313 Pic+maiti Kiongozi CCM wilayani Muleba akutwa amekufa

Wed, 19 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Mwili wa Jaspar Jasson,  aliyekuwa  katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Katoke Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera umekutwa pembeni mwa barabara ukiwa na alama shingoni. Akizungumza leo Jumanne Februari 18, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema alama hizo ni kama za mtu aliyejinyonga. Amebainisha kuwa mwili huo umekutwa katika kijiji cha Bisore wilayani Muleba jana Februari 17, 2020. “Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho ambacho dalili za awali zinaonyesha mauaji yalifanyika eneo tofauti na mwili huo kutelekezwa pembeni mwa barabara,” amesema Kamanda Malimi. Amesema uchunguzi wa awali wa kitabibu umebaini kuwa kifo hicho kimetokana na kukosa hewa. Ameongeza uchunguzi wa daktari umebaini dalili zote za kujinyonga kwa kuwa alikuwa na michubuko shingoni, “pia alikutwa amejisaidia na kujikojolea.” Amewaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi wa kifo hicho kujitokeza.

Chanzo: mwananchi.co.tz