Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

King’ongo waanza kukalia madawati

Bb503c63a30d0a5ec8b85e6cf66c09ab King’ongo waanza kukalia madawati

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAFUNZI wa Shule ya King’ongo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, kesho wataanza rasmi kukaa kwenye madarasa bora na kukalia madawati.

Ofisa Habari wa wilaya hiyo, Joina Nzali amesema hadi sasa shule hiyo imekamilisha kwa asilimia 90 madarasa hayo na kesho wanafunzi wataanza kuingia madarasani.

Amesema madarasa tisa tayari yamekamilika na kuwekwa marumaru na nondo za madirishani. Amesema ujenzi wa matundu ya vyoo 12 unaendelea na utakamilika karibuni.

Baadhi ya wanafunzi hao walikuwa wakisomea chini ya mti, wengine wakikalia matofali na wengine chini kwenye mavumbi.

Rais John Magufuli aliagiza kutatuliwa kwa kero za shule hiyo akiwa mkoani Kagera mwezi uliopita kwenye uzinduzi wa Shule ya Sekondari Ihungo, iliyojengwa upya.

Rais alisisitiza kuwa akirejea Dar es Salaam akute shule huiyo imekamilika, hatua iliyosababisha viongozi wa wilaya ya Ubungo na Mkoa wa Dar es Salaam kukimbizana kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz